Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) lazindua safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Mtwara ambapo ndege aina ya De Havilland Dash 8 - Q400 imetua uwanja wa ndege wa Mtwara na kupewa salamu ya maji “water salute” ikiwa ni ishara ya kuikaribisha.
Akizindua safari hiyo ya kwanza leo tarehe 17 Februari 2025, Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa amelihakikishia shirikika hilo la ndege ushirikiano wa kutosha kutoka Serikali ya mkoa.
“Mtwara ni lango kuu la uchumi wa mikoa ya kusini, niwapongeze ATCL kwa kurejesha safari zake mkoani Mtwara hii itaondoa changamoto za usafiri tulizokuwa nazo kabla ikiwemo suala la bei, hii ni nafuu sana na ndo maana inaitwa nauli za Samia.” Alieleza Mhe. Mwaipaya
Kwa upande wake Rubani kiongozi, Capt. Abdallah Yassin Abdallah ameeleza kuwa wametumia muda wa saa moja kutoka Dar es Salaam mpaka kufika Mtwara. Pia ameeleza uwezo wa ndege hiyo ni kubeba abiria 78 ambapo miongoni mwa abiria waliosafiri kwa ndege hiyo leo ni timu ya mpira ya Simba.
Taarifa ya ATCL imeeleza kuwa shirika hilo litakuwa likifanya safari zake siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kwa bei ya Shilingi 122,000/= kwenda tu na 199,000/= kwenda na kurudi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.