Rekodi ya uzalishaji wa korosho mkoani Mtwara inaelekea kuvunjwa baada ya uzalishaji kufikia tani 171,000. Akizungumza na mwandihsi wetu, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Mtwara Amani Rusake anasema hadi mnada wa 09 uliofanyika Desemba 15, 2017 kwa vyama vyote vya ushirika mkoani hapa, TANECU na MAMCU uzalishaji ulifikia tani 171,000.
Anasema kwa hali ilivyo hana shaka kuwa minada inayofuata, uzalishaji utazidi ule wa mwaka jana. Rekodi ya juu ya uzalishaji wa korosho uliowahi kufikiwa ni msimu wa mwaka jana 2016/2017 ambapo uzalisjhaji ulifikiwa tani 172,681.
Licha ya rekodi ya uzalishaji kuwa juu bado rekodi ya bei ya korosho imeendelea kuvunjwa ambapo kwa musimu huu bei ya juu imefikia shilingi 4055 kwa kilo wakati bei ya chini ikiwa shilingi 3790 Tofauti na rekodi iliyokuwepo ya musimu wa mwaka jana ambapo bei ya juu ilifikia shilingi 4000 kwa kilo wakati bei ya chini ikiwa shilingi 2600.
Wakizunugmzia hali hiyo wananchi wamepongeza serikali ya awamu ya tano kwamba imekuja na muarobaini ambao umesaidia wakulima kuimarisha mashamba yao na hivyo uzalishaji kuongezeka. Wanasema kwa miaka mingi wakulima wa korosho walikuwa wakilalamika serikali kutowajali hali ambayo ilisabisha uzalishaji kupungua.
Katibu wa chama cha Msingi Kusila kijijini Chigweje wilayani Nanyumbu, Sarafina Mohamed anasema sababu kubwa ya ongezeko hili ni kuimarika kwa bei ya korosho hali ambayo imesababisha wakulima kurudi mashambani na kufufua mashamba yaliyokuwa yametelekezwa. Anasema musimu wa mwaka jana aliuza tani 100 lakini mwaka huu hadi mnada wa 08 alikuwa maeuza tani 130. Anasema bado ana matumani ya kupokea korosho zaidi.
Kwa upande wake mkulima maarufu wa korosho kijijini hapo, Lukas Chilonji anasema pamoja na ukweli kwamba kuimarika kwa bei ya korosho ni sababu kubwa ya uzalishaji wa zao hili kuongezeka bado uamuzi wa serikali kuondoa michango mingi iliyokuwa ikiwaumiza wakulima umechangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji kuongezeka.
Maboresho yaliyofanywa na serikali ya wamu ya tano ni pamoja na Utoaji wa pembejeo bure kwa wakulima, kuondoa ushuru wa magunia, pia ushuru wa unyaufu. Hali hiyo Imewafanya wakulima ambao walikuwa hawathamini kilimo cha korosho kuiona thamani yake.
Hata hivyo ameitaka serikali irejeshe utaratibu wa kuchangia pembejeo ili kwa mtu ambaye atashindwa kutoshelezwa na pembejeo inayotolewa bure awe tayari kuchangia kama mfumo wa zamani ulivyokuwa ukifanya. Mfumo huo ulikuwa ukitoa fursa ya wakulima kuchangia nusu ya mahitaji yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.