Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan amepongeza uwekezaji mkubwa uluofanyika mkoani Mtwara. Balozi Avetisyan ametoa pongezi hizo akiwa katika muendelezo wa ziara yake mkoani Mtwara leo tarehe 09 Septemba 2025 ambapo ametembelea kiwanda cha saruji cha Dangote, kiwanda cha kubangua korosho cha Tanecu kilichopo Newala pamoja na mashamba ya korosho.
Akiwa katika kiwanda cha kubangua korosho, Balozi Avetisyan ameeleza nia ya Urusi kupanua soko lake na kununua korosho kutoka Tanzania kwani kwa sasa inanunua kutoka nchi ya Vietnam.
Mwenyekiti wa chama kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU), Bw. Kasim Chipola ametumia fursa hiyo kuomba teknolojia ya utenganishaji wa mabibo na korosho pamoja na pembejeo bora zaidi za mikorosho. Nchi ya Urusi inasafirisha mbolea yake nchi za nje ikiwemo Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.