Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewataka viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kutenga muda wa kwenda kusikiliza kero za wananchi ili kujua changamoto zinazowakabili wananchi na kuzifanyia kazi.
Kanali Sawala amesema hayo kwenye mkutano maalumu wa baraza la madiwani kwa ajili ya kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali mwaka 2022/2023.
Amesema kwa kusikiliza kero za wananchi kutachangia wananchi kuipenda serikali yao na kuendelea kuiunga mkono kwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha Kanali Sawala amewataka viongozi wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Mtwara kusimamia miradi ya maendeleo inayosimamiwa kwenye ngazi za Halmashauri iweze kukamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan analeta fedha nyingi za miradi ya maendeleo lakini kumekuwa na baadhi ya watumishi wachache kutofanya kazi yao ya kusimamia kwa weledi na kusababisha baadhi ya miradi kushindwa kufanya vizuri na kushindwa kukamilika kwa wakati.
Juni 25, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.