• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

MTWARA MWENYEJI WA MAFUNZO YA KOROSHO BARA LA AFRIKA.

Posted on: June 23rd, 2025

Nchi nane za Afrika zimekutana mkoani Mtwara kwa mafunzo ya siku tano kuhusu mnyororo wa zao la korosho yanayojumuisha uzalishaji, ubanguaji, uongezaji thamani, sera, mabadiliko ya hali ya hewa, ushindaji wa korosho bara la Afrika na ulimwenguni kote.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 23 Juni 2025 akifungua mafunzo hayo yanayosimamiwa na African Cashew Alliance amemshukuru na kumpongeza Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kwa kusimamia vema sekta ya kilimo pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyosaidia kilimo cha korosho kwa kutoa pembejeo bure, ajira kwa maafisa ugani na upatikanaji wa masoko ya uhakika.

Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Bw. Alfred Francis amesema Tanzania inashika nafasi ya tano kwa uzalishaji wa korosho duniani na nafasi ya pili kwa Afrika ikiongozwa na nchi ya Ivory Cost.

“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwetu Tanzania kwani tayari tumeanza jitihada za kuinua zao la korosho na mkulima kwa ujumla. Tunajenga kongani la viwanda vya kubangua korosho na maghala kule Maranje, tumeajiri maafisa ugani zaidi ya 500 kwahiyo mafunzo haya yatafanya tupige hatua kubwa zaidi kwenda kwenye mafanikio.” Alisema Bw. Alfred

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Sophia Kashenge alisema “Kwetu korosho ni kila kitu, watu wanaongezeka lakini mabadiliko ya tabia ya nchi yanatuathiri, rutuba katika ardhi inapungua kwa kasi na hii ndo sababu inabidi tushirikiane sote kwa pamoja kuhakikisha mkulima anaongeza uzalishaji”

Katika hatua nyingine imeelezwa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji mkutano wa wa mwaka na maonesho ya 19 ya zao la korosho kwa mataifa ya Afrika, Carribean na Pasifiki utakaofanyika tarehe 18-22 Novemba 2025 ambapo kauli mbiu itakuwa “Wekeza kwenye korosho kwa maendeleo endelevu”.

Nchi zinazoshiriki mafunzo hayo ni pamoja na Tanzania, Kenya, Ghana, Sudan Kusini, Msumbiji, Uganda, Rwanda na Zambia.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SAWALA "ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA"

    June 21, 2025
  • MTWARA MWENYEJI WA MAFUNZO YA KOROSHO BARA LA AFRIKA.

    June 23, 2025
  • NHIF YAFANYA MAZUMGUMZO NA RC SAWALA

    June 23, 2025
  • RC SAWALA AAGIZA VYAMA VYA USHIRIKA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WAKULIMA

    June 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.