Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Ndg. Bwana Eliud Sanga umefika mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ambapo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa mkoa, Mhe. Kanali Patrick Sawala.
Ndg. Sanga, ameeleza lengo la ziara yao ni kuimarisha utendaji kazi wa Mfuko huo mkoani Mtwara ikiwa ni pamoja na kuzungumza na watumishi wa NHIF kuhusu utekelezaji wa majukumu yao, changamoto na mafanikio katika kutoa huduma bora za bima ya afya kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.