Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kusimamia bejeti yake kikamilifu ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza kwenye kwenye mkutano maalum wa baraza la madiwani kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwaka 2022/2023 Kanali Sawala amesema ili kuiwezesha manispaa kujitosheleza katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa vyanzo vya mapato ya ndani.
Aidha amesema kwa miaka mitatu mfululizo Halmashauri ya manispaa ya Mtwara Mikindani imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato yake ya ndani kulingana na bajeti yake iliyopangwa.
Kwa upande wake katibu Tawala wa mkoa wa Mtwara CPA Bahati Geuzye amewataka viongozi hao wa Halmashauri ya manispaa ya Mtwara Mikindani kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia mfumo mpya wa kieletroniki wa manunuzi ya umma-NEST ambao umeanza kutumika katika mwaka wa fedha wa mwaka huu.
Baraza la madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara mikindani imepata hati safi kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 ambapo Mkuu wa Mkoa Kanali Patrick Sawala ameutaka uongozi huo kuendelea kutimiza majukumu yao kwa weledi ili kuendelea kupata hati safi na kuondoa hoja zilizojitokeza, zifungwe na kuacha kutengeneza hoja mpya.
Juni 25, 2024.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.