Na Michael Bakiri - Mtwara RS
MKUU wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brigadia Jenerali Marco Gaguti leo ameongoza wananchi wa Mtwara katika zoezi la chanjo ya UVIKO-19 iliyoanza kutolewa mkoani humo leo Agosti, 3,2021, huku akiwataka wananchi wa Mtwara kuendelea kuzingatia taratitibu zote za kujikinga na ugonjwa huo wa korona kama zilivyo elekezwa na wataalamu wa afya.
Akizungumza mara baada ya kuzindua utoaji chanjo ya Korona ngazi ya Mkoa Brigadia Jenerali Gaguti amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua ya kuruhusu Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ambazo zimepata chanjo ya UVICO-19.
Brigadia Jenerali amesema katika awamu ya kwanza, Mkoa wa Mtwara umepokea chanjo dozi elfu ishirini ambazo kipaumbele kimeelekezwa kwa wahudumu wa afya, watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 50 na watu wenye changamoto ya maradhi kuanzia miaka 18 na kuendelea.
“Mahitaji ya chanjo kwenye Mkoa wetu wa Mtwara ni mkubwa kwani watu takriban 250,000 mpaka sasa wanahitaji chanjo hii hivyo niwaahiahidi kuwa chanjo zaidi zinakuja mkoani Mtwara na kwa wananchi wanaohitaji tutahakikisha wanafikiwa na kuchanja kulingana na mahitaji” Amesema Brigadia Jenerali Gaguti.
Mkuu wa Mkoa pia ameonya waendesha daladala na vyombo vingine vya usafiri kuhakikisha wanachuku tahadhari kwa kuweke vitakasa mikono kwenye magari yao na kuepuka kujaza watu kupita kiasi.
Chanjo hiyo ya UVIKO-19 imeanza kutolewa leo Kwa Halmashuri ya Mtwara na kuanzia tarehe 04 Agosti, 2021 zitaendelea kusambazwa kwenye Halmashari za Mkoa kupitia vituo vya Afya.
Zoezi la uzinduzi wa chanjo limehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya hiyo Dunstan Kyobya, Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Hassan Mtenga, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota, lakini pia viongozi wa Chama pamoja na viongozi mbalimbali wa dini walishiriki zoezi hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.