Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Afya na Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mtwara Wedson Sichalwe akiwasilisha taarifa ya Idara ya Afya wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa na Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kilichofanyika Leo katika Ukumbi Mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara.
Mkuu Wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amefunga mwaka 2017 kwa kupokea mikakati ya utendaji kazi toka kwa wakuu wa Idara na vitengo wa Ofisi Yake. Katika Kikao hicho kilichofanyika leo kwenye ukumbi mdogo Ofisini kwake Mheshimiwa Byakanwa amepokea taarifa za mafanikio na mikakati ya mwaka unaofuata kwa kila Mkuu wa Seksheni na Kitengo na kuwataka kuacha kufanya kazi kwa umoja na mshikamano.
Mheshimiwa Byakanwa ambaye alichaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huu Oktoba 26, Mwaka huu amesema anahitaji kuona Ofisi yake inakuwa na umoja na wote wanafanya kazi kwa ushirikiano. Anasema hiyo ndiyo misingi ya mafanikio ambayo itausogeza mkoa katika lengo lililokusudiwa.
Ameongeza kuwa suala hilo lazima liende na ubunifu wa kiongozi husika badala ya kukaa na kusubiri miongozo na mafungu ya fedha yanayoletwa na serikali. anasema kiongoizi mzuri ni yule ambaye anatumia ubunifu wake kufanikiwa yale yaliyoko katika mipango yake.
Awali wakiwasilisha taarifa hizo wakuu wa Idara wameahidi kufanya kazi katika miongozo na maagizo aliyoyatoa kama kiongozi wao.
Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Renatus Mongogwela amesema Idara imejipanga kufanya mabadiliko mengi ikiwemo kuhakikisha inaitumia tovuti ya mkoa na zile za halmashauri ili kutangaza Mkoa na fursa mbalimbalimbali zilizopo.
Akiitikia mikakati hiyo Mheshimiwa RC ametoa pongezi kwa Afisa Habari wa ofisi yake Evaristy Masuha kwamba anafanya kazi nzuri inayoonekana.
‘Mimi Huwa siyo Mnafiki. Unapofanya jambo jema nakupongeza. Kwa kweli Afisa Habari unafanya kazi nzuri. Unajitahidi kuhuisha taarifa kwa haraka na kwa wakati kwenye tovuti ya Mkoa. endelea na kazi hiyo na ongeza kidogo maboresho niliyoelekeza’ (akimaamisha kutangaza fursa za mkoa ikwemo Bandari ya Mtwara)
Naye Mkuu wa Idara ya Ardhi Mkoa Elias Nyabusani amesema wanatambua migogoro ya ardhi iliyoko hapa mkoani na kwamba wamejipanga kuhakikisha yote inapata ufumbuzi kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu zinazoongoza.
Kutazama video ya tukio husika Bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.