Washiriki wa kozi ya 13 ya ulinzi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) wakiongozwa na Brigedia Jenerali Eric Mhoro leo tarehe 13 Januari 2024 wamefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo kilimo, uvuvi, biashara na maendeleo ya jamii ndani ya mkoa wa Mtwara ili waweze kushiriki vema katika maamuzi ya serikali kwa kila sekta kwa kuzingatia usalama wa taifa.
Brigedia Jenerali Eric Mhoro alieleza kuwa kozi hiyo ina jumla ya wanafunzi 61 kati ya hao 40 ni watanzania na wengine ni kutoka katika nchi 16 ikiwemo Botswana, India, Ethiopia na Misri.
“Suala la ulinzi wa nchi ni la kila mtu na usalama wa kila mwananchi ni muhimu kwa maslahi ya taifa.” Alieleza Bigedia Jenerali Mhoro
Mhe. Kanali Patrick Sawala, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewahakikishia ushirikiano kwa kipindi chote watakachokuwa mkoani hapa kwa mafunzo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.