Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 04 Aprili 2025 amekabidhi vitendea kazi kwa Jeshi la polisi na Idara ya Uhamiaji ambavyo vimetolewa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na Taasisi ya Search for common ground.
“TPDC wamekuwa na utaratibu mzuri wa kurudisha kwa jamii kile wanachokipata (CSR), kwa Jeshi letu la polisi walijenga kituo pale Msimbati, ilibakia samani ili kianze kufanya kazi. Nimshukuru Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati, Mhe. Dotto Biteko kwa maelekezo yake na sasa yamefanyiwa kazi.” Alieleza Kanali Sawala
RC Sawala ameishukuru Taasisi ya Search for common ground kupitia mradi wake wa “Daraja la Amani” wenye lengo la kuimarisha biashara zinazovuka mipakani sambamba na kuimarisha maendeleo katika jamii za mipakani.
“Nimshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia maboresho ya Jeshi la Polisi katika nyanja zote, pia niwashukuru TPDC kwa ufadhili wao kwani kabla ya ya ufadhili huu wa vifaa vya leo tayari wametujengea kituo chenye thamani ya zaidi ya Milioni 186 na wametuahidi kutijengea nyumba ya Mkuu wa kituo na za askari, hii itakuwa chachu ya utendaji wetu sisi polisi pale Msimbati.” Alieleza SACP Issa Selemani, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewataka Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kushirikiana vema na vyombo vyote vya ulinzi na usalama ili waweze kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kimaendelea katika mazingira rafiki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.