Katibu Tawala mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye amezitaka Taasisi za serikali zinazodaiwa na wazabuni mbalimbali kuweka mikakati ya kuhakikisha wanalipa madeni hayo. CPA. Geuzye ametoa rai hiyo leo tarehe 27 Juni 2025 wakati wa kikao kulichofanyika ukumbi wa Boma, kilichowakutanisha wazabuni na Taasisi za serikali zinazodaiwa.
“Dawa ya deni ni kulipa, tunafahamu tuna ufinyu wa rasilimali lakini ni busara kutenga bajeti kulipa kidogo kidogo ili wazabuni waendelee kutoa huduma bora. Tujiulize sisi tukiwa tunaenda kazini halafu hatulipwi, ingekuwaje?” Alihoji CPA. Geuzye
Mkuu wa kitengo cha manunuzi mkoa wa Mtwara, Bi Theresia Nsanzugwako ametoa wito kwa wazabuni wanaofanya kazi na Taasisi za serikali kuhakikisha wanafuata taratibu za ofisi ikiwemo kusaini mikataba na wakuu wa Taasisi ili hata ikitokea mtu hayupo ofisini nyaraka ziwepo na madeni yawe na sifa ya kulipika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.