Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba amepiga marufuku michango inayokwenda kinyume na maagizo yaliyoko katika miongozo ya elimu shuleni. Agizo hilo amelitoa jana Februali 24, 2020 kufuatia malalamiko ya wananchi wakati wa ziara yake ya siku moja kusikiliza kero za wananchi na kukagua maendeleo ya shule. Wananchi hao walidai kuwa baadhi ya shule hasa za sekondari walimu wamekuwa wakiomba michango ambayo inaleta usumbufu kwa wazazi. Mheshimiwa Walyuba amesema michango inayokwenda kinyume na utaratibu inaweza kuwa chanzo cha wanafunzi kushindwa kuhudhuria shuleni na kwamba inapingana na dhana ya elimu bila malipo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano kupitia kwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Bonyeza HAPA kupata picha na maelezo zaidi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.