Viongozi wa taasisi za serikali mkoa wa Mtwara wakifuatilia mada juu ya haki na wajibu wa EWURA kwa wateja wa Nishati na maji iliyokuwa ikitolewa na Meneja mawasiliano kwa Umma, Titus Kaguo leo April 11, 2019 (hayupo pichani) katika ukumbi wa Chuo cha Veta Mtwara
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewataka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kuhakikisha wanatoa elimu kwa Umma ili kuhakikisha jamii inatambua wajibu na haki zao katika huduma zinazotolewa Mamlaka hiyo.
Agizo hilo amelitoa wakati akifungua Semina elekezi juu ya wajibu wa (EWURA) katika Ukumbi wa VETA Mtwara April 11, 2019. Semina hiyo ililenga kuwajengea ufahamu viongozi wa Mkoa wa Mtwara juu ya shughuli zinazofanywa na EWURA.
Amesema wananchi wanayo maswali mengi yasiyo na majibu hivyo EWURA wanajukumu la kuhakikisha wananchi hao wanapata ufahamu.
Kwa upande wake Meneja mawasiliano kwa umma, EWURA makao makuu Titus Kaguo amesema mamlaka imejipanga kuhakikisha jamii inafikiwa. Amekili kuwepo na changamoto ya uelewa juu ya haki za wananchi katika huduma za Nishati na Umeme na wamekwua wakijitahidi kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo redio na Televisheni. Amewataka viongozi kutoa ushirikiano kwani wao ndio wako karibu zaidi na jamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.