Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed Leo hii Feb 19, 2024 akabidhi vifaavya TEHAMA kwa vituo 10 vya walimu (TRC) kupitia Mradi wa Boost ambapo amesema nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuiona siku ya leo na kuweza kufanikisha hafla hii ya kukabidhi kompyuta 50, printa 10 na UPS 30 vituo vya walimu/shule teule 10, hafla ya makabidhiano haya yanawakilisha Halmashauri 9 za Mkoa wa Mtwara zenye jumla ya walimu wa Shule zaMsingi 5,129 na Shule za Sekondari 2,457.
Kupitia hotuba yake amesema Napenda kuwapongeza walimukwa matokeo mazuri ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2023. Jumla yawanafunzi 28,107 sawana asilimia 79 wamefauluna kuchaguliwa kujiunga na shule za sekondari mwaka 2024. Kiwango hiki cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 3 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2022 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 76.
Pia Kanali Ahmed ametumia fursa hiyo kuwapongeza wazazi/walezi, walimu, Maafisa Elimu Kata, Maafisa Elimu ngazi ya Halmashauri pamoja na viongozi wa Wilaya zote kwa jitihada mnazozifanya katika kuhakikisha kwamba hali ya ufaulu katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi inaimarika kila mwaka.
Hali kadhalika Mkuu wa Mkoa akasema mapokezi ya vifaa hivi vitasaidia katika kuwawezesha walimu kujifunza mbinu mbalimbali zaufundishaji na ujifunzaji kupitia Mpango Endelevu wa Mafunzo ya Walimu Kazini (MEWAKA), mafunzo yanayofanyika ngazi ya Shule na Klasta.
Vifaa hivi vitawezesha upatikanaji wa nakala laini za vitabu vya kiada na ziada, kuzalisha mitihani na majaribio mbalimbali. Kufanya uchambuzi wa matokeo ya Mitihani na kuhifadhi katika nakala laini.
Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunatakiwa kuhakikisha vifaa hivi vinavyokabidhiwa leo vinatumika kikamilifu nakutunzwa.
Katika Kuhitimisha hutoba yake Kanali Ahmed akasema napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza walimu wote kwa jitihada kubwa mnayoifanya katika kuhakikisha tendo la ufundishaji na ujifunzaji linatekelezwa ipasavyo katika Mkoa wetu.
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.