HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA WA USANIFU NA UJENZI WA JENGO LA ABIRA, VITUO VYA ZIMAMOTO, HALI YA HEWA PAMOJA NA MNARA WA KUONGOZEA NDEGE KATIKA KIWANJA CHA NDEGE MTWARA.
Serikali imeisaini mkataba wa shilingi bilioni 73.5 na Mkandarasi kwa ajili ya usanifu na ujenzi wa jengo la abiria, vituo vya zima moto na Hali ya hewa pamoja na mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege Mkoani Mtwara.
Mkataba huo umesainiwa leo tarehe 29 Mwezi Aprili , 2024 na Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Ibrahim Mbura na Mkandarasi wa China Railway Engineering Company Group.
Hafla ya utiaji saini imeshuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala na viongozi wengine wa kitaifa wakiwemo wabunge katika uwanja mpya wa Ndege Mkoani humu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Mbarawa amesema fedha ya utekelezaji wa mradi ipo na kwamba tayari Mkandarasi yupo saiti kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.
"Mkandarasi ana uwezo mkubwa na hatuna shaka kazi itamalizika kwa viwango na kwa wakati uliopangwa," amesema na kuongeza kuwa mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 36.
Mkuu wa Mkoa Kanali Patrick Sawala ameishukuru Wizara ya Uchukuzi kwa kuendelea kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu ujenzi wa miradi ya maendeleo Mkoa wa Mtwara.
Aprili 29, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.