Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Renatus Mongogwela
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Renatus Mongogwela amewataka Wakurugenzi wa halmashauri na washiriki kupokea changamotoza utekelezaji wa shughuli za Mradi wa Tusome pamoja na kuzifanyia kazi.
Ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa mradi wa Tusome pamoja uliofanyika katika ukumbi wa Naff BeachHotel mjini Mtwara
Amesisitiza kuwa kwa miaka ya hivi karibuni Mkoawa Mtwara umekuwa ukijivunia mafanikio katika mitihani ya darasa la Nne na laSaba kutokana na shughuli nzuri inayofanywa na Mradi.
"Mafanikio ya Mkoa katika mitihani yakitaifa ni kutokana na uwepo wa mradi. Rejeeni matokeo ya darasa la Nne naDarasa la saba mwaka 2018 ambapo mkoa ulikuwa wa Nne kitaifa. Ndugu zangulitakuwa kosa kubwa kama tutashindwa kuundeleza mradi huu. " Amesema.
Mradi wa Tusome pamoja ulianzishwa mwaka 2016chini ya ufadhili wa Watu wa Marekani (USAID) na unatarajia kufikia mwisho januari2021 huku ikitarajiwa Mkoa kuuendeleza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.