Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara imeibuka mshindi wa kwanza wa maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini mwaka 2018 kati ya halmashauri 15 za Mikoa ya Lindi na Mtwara zilizoshiriki maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Mbali na kuwa mshindi wa kwanza kwa upande wa halmashauri, Halmashauri hiyo imekuwa mshindi wa pili wa jumla katika kilele cha maonesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutoa maarifa ya kilimo bora kwa wakulima.
Akizungumzia vigezo vilivyotumika katika kumpata mshindi wa maonesho hayo, Mratibu wa maonesho hayo ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Sekretarieti ya mkoa wa Mtwara Amani Rusake amesema Ushindi huo umetokana na banda hilo kuweza kutafsiri kwa vitendo kauli mbiu ya maonesho hayo ya “Wekeza katika Kilimo mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda” ambapo teknologia za kisasa zilioneshwa katika mashamba darasa ikiwemo faida za matumizi sahihi ya Pembejeo kama mbegu za kisasa na viwatilifu ili kuwa na uzalishaji wenye tija utakaopelekelea viwanda kuwa na malighafi za kutosha.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Masasi iliweza kuonesha kilimo jumuishi ambapo watu wenye ulemavu wanaweza kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi kupitia shughui za kilimo cha bustani wakiwa nyumbani kwa kutumia vifaa rahisi kama makopo, mifuko mataili na vitu vingine ambapo wanaweza kuhudumia kwa urahisi bila kwenda mashamba ya mbali.
Halmashauri imeibuka kidedea baada ya kukidhi vigezo vya kuwa banda bora kwa kuonesha teknolojia za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa vitendo.
soma habari nzima na picha kwa kubonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.