Msanii wa Bongo Fleva Rajab Abdul Kahali maarufu kama 'Haromonize' ametua Mjini Mtwara Tayari kuungana na wakazi wa mji wa Masasi kutangaza utalii wa mji huo kupitia mlima Mkomaindo. Harmonize ambaye ametua na kundi la wasanii kutoka nje na ndani ya Tanzania amesema lengo lake ni kuhakikisha sanaa ya kusini inainuka na hivyo kufikia ndoto yake ya kuhakikisha analipa fadhila kwa heshima aliyopewa na watu wa Kusini.
"Nimeona si vema hili tamasha la nyumbani kuja mimi Peke yangu. ninawashabiki wengi nje na ndani ya Tanzania hivyo nimeamua kuja na wasanii wengine kutoka nje ya Tanzania ili wanaMtwara waige kwangu na kwa wasanii hawa". Amesema Harmonize.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amempongeza Harmonize kwa kuwa tayari kuhudhuria tamasha hilo. Amesema uwepo wake utaongeza hamasa na kulifanya tukio lifanikiwe zaidi.
Amesisitiza kuwa lengo lake ni kuhakikisha fursa za utalii kwa mikoa ya kusini inatangazwa zaidi ili kuwavutia watalii na kuinua uchumi wa mkoa.
Tamasha la Masasi Rock Festival linatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 6-9, 2019 huko Masasi`. Tamasha hili ambalo linakusudia kutangaza fursa ya utalii kupitia mlima Mkomaindo litahusisha michezo mbalimbali pamoja na kupanda kwenye kilele cha mlima huo`
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.