Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, Liberatus Sabas
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama Vimeimarisha ulinzi katika mipaka ya Tanzania ili kuhakikisha wahalifu wanaofanya mauaji na vurugu nchini Msumbiji hawapati nafasi ya kuingia Tanzania.
Hayo yamesemwa leo na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Liberatus Sabas wakati akikagua kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu nchini kilichowasili mkoani Mtwara kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
Amesema wahalifu hao wamekuwa wakivamia kambi za jeshi, vituo vya polisi, kuchoma moto na kuchukua silaha nchini Msumbiji na pia wameripotiwa kuvamia benki na kupora fedha huko huko Msumbiji.
“Kule hali si shwali kama ambavyo mmekuwa mkisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Sisi kwa kutambua hilo, na kutambua umuhimu wa sisi kama Taifa, na umuhimu wa wananchi wa Tanzania kuwa shwali tumejipanga kuhakikisha tatizo hili haliji huku kwetu.”
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwasilisha taarifa za mtu yeyote ambaye wanamtilia shaka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.