Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Patrick Sawala amelitaka Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Mtwara kuendelea kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wananchi juu ya kubiliana na majanga mbalimbali pia watumie fursa zinazipatikana kuandaa klabu za kutoa elimu ya majanga ya moto.
Akuzungumza leo Juni 30,2025 katika kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa jeshi hilo kwa mwaka 2024/2025 kilichofanyika ukumbi wa Tiffany mkoani mtwara. Mhe. Sawala amelisihi jeshi la zimamoto na uokoaji kuendelea kusimamia sheria ipasavyo.
Aidha Mhe. Sawala amewasihi watumishi hao wa Jeshi la zimamoto na uokoaji kutojihusisha na siasa na badala yake wafanye kazi.
Kikao hicho kilibeba kaulimbiu ya “Okoa maisha na mali, piga 114”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.