Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema njia pekee itayolisaidia Taifa kwenda sambamba na mabadiliko ya teknoloji, mifumo ya Maisha na mabadiliko ya uchumi wa dunia ni kuhakikisha serikali inaandaa mpango mahususi utakaoiwezesha kukabiliana na mabadiliko yatakayojitokeza.
Kanali Abbas ametoa kauli hiyo wakati akifungua Semina ya siku moja iliyolenga kuwajengea uwezo wadau mbalimbali kuhusu maandalizi ya Dira ya taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 katika ngazi ya Mkoa huku akisisitiza kuwa kutokana na kasi ya mabadiliko katika Kila nyanja ni lazima Serikali iwaandalie Wananchi wake mazingira wezeshi kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya aina yeyote.
“Ndugu zangu washiriki wa semina hii, bila shaka kila mmoja wenu ni shuhuda wa mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanatokea kila uchwao, hii inadhihirisha kuwa Kuna uwezekano miaka 25 ijayo kutakuwa na mabadiliko makubwa zaidi ya haya tunayoyaona , hivyo ni lazima tujiandae kuyakabili” alisema Kanali Abbas.
Aidha Kanali Abbas ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kuanza kuiandaa jamii na wadau mbalimbali kwa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 na kusisitiza kuwa utaratibu huo utasaidia kupunguza maswali.
MWIISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.