Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ameziagiza Halmashauri za Mkoa wa Mtwara kukamilisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ifikapo juni 30, 2025.
Kanali Sawala ametoa rai hiyo mapema Leo 13 juni, 2025 Katika ukumbi wa Tutzing ndanda , Masasi ambapo amesisitiza kuwa Serikali ya mkoa itahakikisha inaelekeza nguvu zake zote kusimamia miradi ya maendeleo, ambayo Serikali imetoka mabilioni ya fedha kuitekeleza , huku akiwapa wiki 2 watendaji Katika halmashauri kukamilisha kazi hiyo.
" Ndugu wakuu wa wilaya, wakurugenzi na watumishi wote ndani ya halmashauri ninawaagiza ifikapo Juni 30,2025 miradi yote iwe imekamilika, inyeshe mvua liwake jua tengeni muda wa ziada, simamieni Kwa karibu fedha mlizoletewa na serikali , mkifanya hivyo mtakuwa salama " alisema Kanali Sawala
Halikadhalika Kanali Sawala amewataka Viongozi na watendaji wote Katika ngazi ya wilaya na halmashauri kutimiza wajibu wao kikamilifu, ikiwemo kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mpaka kukamilika kwake ,hatua ambayo amesema itawapunguzia adha wananchi wake.
"Ndugu Viongozi na watendaji mlioko hapa Kwa namna moja au nyingine kila mmoja wenu anawajibu kuhakikisha fedha inayoletwa na serikali kutekeleza miradi ya maendeleo inatumika kama ilivyo kusudiwa, hivyo nendeni mkahakikishe adhima ya Serikali inatimia. alisisitiza Kanali Sawala
Katika ziara hiyo ya Siku nne Kanali Patrick Sawala akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa amekagua jumla ya miradi 12 ya ujenzi wa miundombini ya elimu iliyo gharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.6.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.