BANDARI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imesema serikali ilifanya jambo la muhimu kuwekeza pesa nyingi katika kuboresha miundombinu ya Bandari ya Mtwara.
Akiongea mara baada ya kamati hiyo kutemebelea bandari hiyo leo tarehe 25 Machi 2024, Mwenyekiti wa kamati hiyo Deus Sangu amesema uwekezaji huo umekuwa na tija kubwa kibiashara katika bandari hiyo.
"Jambo kubwa na la muhimu ambalo serikali ilifanya na limeleta faida kubwa ni uwekezaji wa shilingi takribani bilioni 157 katika Bandari hii ya Mtwara, uwekezaji huo umeleta mapinduzi makubwa,".
Akitoa taarifa ya maendeleo ya Bandari hiyo, Naibu Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Mhandisi Juma Kijavara amesema uwekezaji huo umeiwezesha Bandari kuhudumia shehena za tani milioni 1.1 mizingo na kuvuka lengo.
Kabla ya uwekezaji huo (Shilingi bilioni 157) Bandari hiyo ilikuwa na uwezo wa kuhudumia tani 400,000 tangu ilivyojengwa mwaka 1954.
Kwa mujibu wa taarifa, kipindi cha mwaka 2022/2024 Bandari ya Mtwara ilihudumia mizigo tani 1,126,300 na kuvuka lengo la kusafirisha tani 1000,000.
Kijavara amesema bandari iliweka lengo la kusafirisha tani milioni 1.2 kufika mwaka 2025 ambapo lengo hilo limefikwa kabla ya kipindi husika.
Kwa hatua nyingine, kamati hiyo imetoa wito kwa serikali kuboresha miundombinu ambayo inaunganisha bandari ya sehemu mbalimbali ikiwemo Ruvuma ambapo kunafanyika uchimbaji wa makaa ya mawe ambayo yanasafirishwa kwenda nchi za nje kupitia Bandari ya Mtwara.
Machi 25, 2024
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.