Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Ccm Mkoa wa Mtwara Said Nyengedi amewahakikishia watumishi katika sekta ya Afya Wilayani Nanyumbu kuwa Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuweka mazingira rafiki katika maeneo ya kazi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Akizungumza na watumishi wakiwemo wauguzi na madaktari katika hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya mkoa iliyolenga kukagua miradi ya maendeleo , Bw Nyengedi amesema kuwa tayari serikali imeanza kuzipatia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazo ikabili Sekta ya afya ikiwemo uhaba wa watumishi.
“Ndugu wauguzi na madaktari mliopo hapa bila shaka ninyi wote ni mashaidi kuwa Mhe. Dkt Rais Samia Suluhu Hassani anaupenda sana Mkoa wetu maboresho yote mnayo yashuhudia katika hospitali yetu ya Wilaya ni ishara tosha ya upendo kwetu” alisema Bw Nyengedi
Katika ziara hiyo ya kamati ya siasa ya mkoa iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. kanali Patrick Sawala Bw Nyengedi alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Mkoa kwa usimamizi makini wa miradi ya maendeleo hatua ambayo amesema anawatia moyo wananchi kuendelea kuiamini Serikali yao.
“Mwenye macho haambiwi tazama , hivi punde nimemaliza kukagua miundombinu ya sekondari kilimanihewa kwa ujumla nimeridhika kwa hatua iliyofikiwa, niwasihi wazazi ifikapo Januari 13 waruhusuni watoto waanze masomo” alisisitiza Bw Nyengedi.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala amemuhakikishia Comredi Nyengedi kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kusimamia kwa uadilifu Fedha zote zinazoletwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.