Kampeni ya SHULE NI CHOO MSITIRI MWANAFUNZI NA MWALIMU iliyoanzishwa na mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa imekusanya zaidi ya shilingi milioni 265. Kampeini hiyo ilitangzwa mapema Agosti mwaka huu na Mkuu wa Mkoa huo na kuzinduliwa leo na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
Akitambulisha kampeni hiyo Byakanwa amesema Mkoa una upungufu wa matundu ya choo 6,674 ambayo gharama za ujenzi zinafikia bilioni 6,674,000,000.
Byakanwa ambaye amekuwa akitambulisha kipaumbele chake cha kwanza kuwa ni elimu amesema Gharama hizo hazimtishi kwani wananchi anaoongoza wanaonesha mwitikio mzuri na wako tayarikushiriki kwa njia moja ama nyingine kupunguza gharama hizo.
Kwa upande wake Mgeni rasmi wa uzinduzi huo Mhe. Profesa joyce Ndalichako amepongeza hatua hiyo na kusema itasaidia kuongeza hamasa ya kusoma na kupunguza maradhi kwa wanafunzi na walimu. Amesema Wizara yake itachangia shilingi milioni mia moja na kumi.
Wachangiaji wengine waliojitokeza katika kampeni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja ni pamoja na Wizara ya Afya, wafanyabiashara, vyama vya wafanyakazi na makampuni binafsi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.