Kampeni ya Shule ni choo inatarajiwa kuzinduliwa mkoani Mtwara September mwaka huu. Kampeini hii itakayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja itawahusisha waliowahi kusoma mkoani mtwara kuchangia ujenzi wa choo kwenye shule walizosoma.
Akitangaza kampeni hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amesema lengo ni kuwashirikisha watanzania kuchangia maendeleo ya shule walizosoma.
“Hatuoneshi kwenye vyombo vya habari kumdhalilisha mtu bali kumuonesha hali ilivyo kwenye shule aliyosoma, huku tukitambua kuwa hiyo shule ambayo haina hali nzuri, ndiyo iliyomfanya afike hapo alipo”.
Byakanwa amesema upungufu wa matundu ya choo kwa mkoa wa mtwara ni 6,674 ambapo thamani yake ni shilingi Bilioni 6 na milioni mia sita sabini na nane. Matundu yaliyopo kwa sasa ni 5,747 wakati mahitaji ni matundu 11,422.
Kwa upande wa walimu upungufu ni matundu 1864 yenye thamani ya shilingi bilini 1 na milioni mia nane sitini na moja.
Amesema kampeini hii itaanza kwa kutambua watu mbalimbali walioko ndani na nje ya Mkoa wa Mtwara ambao walisoma kwenye shule hizo. Hatua ya pili ni kuonesha hali ya vyoo katika shule hizo kupitia vyombo vya habari na kuwataka waliosoma katika shule hizo wachangie ujenzi wa shule hizo.
Amesisitiza kuwa mkoa hauhitaji kupokea hizo fedha bali wasomi hao wanaweza kuchangia kwa kutumia utaalamu wao.
kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa, Germana Mung’aho amesema upungufu huo unachangia katika watoto kutofanya vizuri. Amesema elimu haiishii kujifunza darasani bali ni pamoja na mazingira yanayomzunguka mwalimu na mwananfunzi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.