Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda leo August 16, 2018 amezindua rasmi kampeni ya upimaji wa maambukizi ya UKIMWI kwa wananchi waishio Mkoani Mtwara.
Kampeni hiyo ambayo inasimamiwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation ina lengo la kuhamasisha wananchi waishio Manispaa ya Mtwara-Mikindani pamoja na wale waishio Halmashauri ya Mji wa Masasi hususani wanaume kujitokeza kwenye upimaji wa virusi vya UKIMWI na kuanza kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi kwa wale wote watakaokutwa na maambukizi.
Pamoja na upimaji wa virusi vya UKIMWI kutakuwana upimaji wa magonjwa mengine kama Malaria, shinikizo la damu, sukari namagonjwa mengine.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyoinayoenda na kaulimbiu isemayo "FURAHA YANGU, PIMA, JITAMBUE, ISHI" Mkuuwa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Mmanda ametoa wito kwa wananchi wote kujitokezakwa wingi kwenye upimaji ili kutambua afya zao na kuchukua hatua.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.