Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala Leo Julai 9, 2024 amekabidhi magari 3 yenye thamani ya shilingi Zaidi ya Milioni 600 Kwa wakuu wa Wilaya za Mtwara, Tandahimba na Newala.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya magari hayo iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kanali Sawala amesema magari hayo yatasaidia kuongeza tija katika ufuatiliaji na usimamizi wa miradi ya Maendeleo.
Aidha Kanali Sawala amewaagiza wakuu wa Wilaya waliokabidhiwa magari hayo kuyatumia kikamilifu kuwatembelea wananchi na kusikiliza kero zao na kuzipatia majawabu.
Halikadhalika Kanali Patrick Sawala pia amewataka maafisa usafirishaji waliopokea magari hayo kuyatunza na kuyafanyia matengenezo ya mara Kwa mara Ili yaweze kudumu.
Pia Kanali Sawala ameitumia hafla hiyo kumshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwajali Wanamtwara hatua ambayo amesema itasaidia kuongeza kasi ya Maendeleo.
Julai 9, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.