Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Kenan Sawala Mapema leo hii aongoza kikao cha Mfumo wa Usafirishaji wa Dharula kwa Akina Mama na Watoto wachanga chini ya siku 28 (M-MAMA)
Akiwa katika kikao hicho amesema, Serikali inayo dhamira ya dhati kabisa ya kuboresha huduma za afya ya uzazi na watoto hapa nchini na kumaliza tatizo la vifo vitokanavyo na uzazi na Vifo vya watoto wachanga.
Aidha Mfumo huu ulizinduliwa rasmi kitaifa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tar 6/4/2022 na mikoa yote Tanzania ilizindua kwa wakati tofauti ambapo Mkoa wetu wa Mtwara Tulizindua rasmi tar. 22/12/2023 na mfumo kuanza kufanya kazi tar 1/4/2024 baada ya kupitia hatua kadhaa za kujenga uwezo kwa taasisi zetu kwa kuweka vifaa vya mawasiliano na utunzaji wa kumbukumbu katika chumba cha uratibu na mawasiliano kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula na kuendesha mafunzo kwa watumishi pamoja na madereva wa jamii waliokubali kufanya kazi ya kusafirisha wagonjwa.
Kanali Sawala akaongeza kuwa, Serikali imefanya juhudi kubwa za kuleta magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ili kuimarisha huduma za rufaa za wagonjwa na hasa mama na mtoto. kwa sasa Mkoa una jumla ya Ambulance 32 ambapo kati ya hizo 13 ni mpya kabisa.
Kabla ya kuhitimisha hotuba yake Kanali Sawala akasisitiza kwamba, rufaa kwa wazazi na watoto wachanga ni jambo la kila mmoja wetu, na ni wajibu wa kila Halmashauri kusimamia mfumo wa M-MAMA kwa kuhakikisha magari ya wagonjwa yako tayari wakati wote na pia zihakikishe kuna ushirikiano mzuri wa madereva jamii pale ambapo Ambulance haitaweza kufanikisha rufaa hizi
Kanali Sawala amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ifuatavyo;
Kuendelea kuweka fedha kwenye akaunti ya M-MAMA iliyoanzishwa na Serikali.
Kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya magari ya wagonjwa.
Kutoa kipaumbele katika kuidhinisha malipo ya dereva Jamii kwa wakati.
Julai 5, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.