Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego amewaongoza wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuupokea Mwenge wa uhuru huku akiahidi kuukimbiza umbali wa kilometa 871.7 mkoani Mtwara kwa amani na utulivu.
Akizungumza katika tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Ngwale kilichopo wilayani Nayumbu ulikopokelewa Mwenge huo leo, amesema Mwenge huo ambao ni tunu ya taifa utazindua, kukagua, kufungua na kuweka Mawe ya Msingi kwenye miradi 55.
Ameitaja thamani ya miradi hiyo kuwa ni shilingi 17,736,208,216 ambapo mchango wa wananchi ni shilingi 1,806,008,400 sawa na asilimia 10.2. Mchango wa halmashauri shilingi 2,541,256,295.6 sawa na asilimia 14.5. Mchango wa Serikali Kuu shilingi 8, 040,242,267 sawa na asilimia 45.3 wakati mchango wa wahisani ni shilingi 5,348,698,298 sawa na asilimia 30.2
Dendego amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Mtwara kutoa ushirikiano Wakati mwenge utakapokuwa ukipita kwenye maeneo yao.
Awali akiwaaga wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour Amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ….kuhakikisha anaongeza nguvu katika kuimarisha miradi iliyozinduliwa. Ameitaja moja ya changamoto kubwa waliyoishuhudia katika Mbio hizo kuwa ni pamoja na mapungufu mengi katika miradi ya maji.
Amesema baadhi ya miradi ya maji iliyopitiwa na Mwenge haikuwa katika kiwango kizuri cha ubora hivyo wahakikshe wanaongeza nguzu ili wananchi waweze kuona manufaa ya ujio wa Mwenge katika maeneo yao.
Aidha Kiongozi huyo amewataka viongozi wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia na kulinda uhuru wa vyombo vya habari pasipo kuzuia utoaji wa taarifa. Amesema zipo taarifa za kuzuia baadhi ya taarifa zisitolewa na waandishi wa habari jambo ambalo linawanyima wananchi uhuru wa kupata habari.
Mwenge wa Uhuru 2017 utakimbizwa kwa siku 10 mkoani hati tarehe 21 utkapokabidhiwa kwa uongozi wa mkoa wa Lindi katika kijiji cha
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.