Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Gasper Byakanwa akizungumza na Waalimu wa shule za Msingi na Sekondari wa Wilaya ya Tandahimba katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wakati wa ziara yake ya kujitambulisha wilayani hapo.
Na. Edwin Ekon. Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
KIFUPI: YALIYOJIRI KATIKA ZIARA YA KUJITAMBULISHA MKUU WA MKOA WA MTWARA MHE.GALASIUS GASPAR BYAKANWA WILAYANI TANDAHIMBA:
Pichani: Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Galasius Gaspa Byakanwa akizungumza na Waalimu wa shule za Msingi na Sekondari wa Wilaya ya Tandahimba katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wakati wa ziara yake ya kujitambulisha wilayani humo aliyoifanya leo tarehe 17.01.2018
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Galasius Gaspar Byakanwa amefanya ziara ya kujitambulisha kwa wananchi, watumishi na viongozi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Mhe. Mkuu wa Mkoa katika ziara yake alishiriki zoezi la kupanda miche ya mikorosho katika shamba darasa lililopo katika Kata ya Nanhyanga, pia amezungumza na watumishi wa kada mbalimbali za serikali kuu na serikali za mitaa pamoja na walimu wa shule za msingi na Sekondari zilizopo wilayani Tandahimba.
Akiwa katika zoezi la kupanda miche ya mikorosho, Mhe. Byakanwa amewataka wakulima kupanda miche mipya na bora ya mikorosho kwa mfumo wa kuchanganya aina tofauti tofauti za miche ya mikorosho ili kuwawezesha kujua ni aina gani ya mikorosho ni bora zaidi kuliko mingine ili kuongeza uzalishaji wa zao la korosho.
YALIJIRI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI:
►Halmashauri isimamie zoezi la kupima viwanja kwa lengo la kuboresha mji kwa kuzingatia matumizi bora ya ardhi na sio kujali mapato pekee, Aidha upimaji wa ardhi uzingatie maeneo ya Maziko, Taasisi mbalimbali za Umma, maeneo ya wazi. Ametoa rai kwa Wahe. Madiwani kusimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa na Halmashauri ili iendane na thamani ya fedha za serikali.
►Amesisitiza suala la amani, utulivu na mshikamano kwa kueleza kuwa mkoa wa Mtwara haupo salama sana kutokana na vikundi vya kigaidi kutoka nchi jirani ya Msumbiji wakishirikiana na baadhi ya watanzania. ametoa rai kwa Watendaji wa vijiji kuwa wenyeviti wa ulinzi na usalama katika maeneo yao, Aidha ameagiza kuanzisha daftari la wakazi katika kila kijiji kwa lengo la kujua takwimu pamoja na kujenga msingi wa kufahamiana ambapo mwisho wa zoezi hilo ni mwezi Machi,2018 takwimu zipatikane.
►Amewakumbusha wakulima kutobweteka na zao la korosho pekee, amewataka kulima mazao mengine ya chakula ili kuondokana na tatizo la njaa. Aidha, amewataka wakulima kuongeza kasi ya kulima zao la korosho kwani kuna maeneo mengine yameanza kulima zao hilo.
►Katika kuboresha afya za wananchi wanaonufaika na Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF), ameagiza wanufaika wote kuchangia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kupitia fedha wanazopata na zoezi hilo liwe limekamilika mwisho wa mwezi huu.
YAFUATAYO YALIJIRI KATIKA MAZUNGUMZO NA WAALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI:
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Galasius Gaspar Byakanwa amesikitishwa na kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za wilaya ya Tandahimba kwa kushika nafasi zisizoridhisha kitaifa; hivyo ametoa maagizo yafuatayo ili kuboresha hali ya ufaulu wa wanafunzi katika Mkoa wa Mtwara:
►Kuanzisha vibao vitakavyoonesha wanafunzi waliofaulu vizuri na walimu waliofaulisha
Katika agizo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewataka wakuu wa Shule za msingi na Sekondari kuwa na utaratibu wa kuanzisha kibao kitakachoonesha wanafunzi waliofaulu vizuri pamoja na walimu waliofaulisha masomo husika ili kuleta ushindani kwa wanafunzi pia kuleta ari ya kufundisha kwa walimu. Pia kuwa na kumbukumbu na kuwathamini wanafunzi na waalimu wanaofanya vizuri.
►Kuwa na malengo kuanzia ngazi ya shule, kata hadi wilaya
Katika agizo hilo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameagiza halmashauri kuhakikisha shule zote za msingi na sekondari zinakaa pamoja kuweka mbinu za kufikia malengo ya shule, kata na hata wilaya katika kuinua hali ya ufaulu Mkoani Mtwara, “ Bila malengo hatuwezi kufika popote” Alisisitiza.
►Suala la kumaliza Mtaala wa masomo (Syllabus)
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewataka waalimu wote wa shule za msingi na Sekondari ambao wanafundisha madarasa ya mitihani (Yaani darasa la Nne na Saba kwa shule za msingi na Kidato cha Pili na Nne kwa shule za Sekondari) kuhakikisha wanamaliza Mtaala wa masomo yao (Syllabus) ifikapo mwezi Juni na baada ya hapo wahakikishe wanawafanyisha mitihani mitatu yenye hadhi ya mitihani ya kitaifa ili kuwajengea uwezo na utyari wanafunzi katika mitihani yao ya taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Galasius Gaspar Byakanwa amekerwa na kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za wilaya ya Tandahimba kwa kushika nafasi zisizoridhisha kitaifa; hivyo ametoa maagizo yafuatayo ili kuboresha hali ya ufaulu wa wanafunzi katika Mkoa wa Mtwara:
►Kuanzisha vibao vitakavyoonesha wanafunzi waliofaulu vizuri na walimu waliofaulisha
Katika agizo hilo,Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewataka wakuu wa Shule za msingi na Sekondari kuwa na utaratibu wa kuanzisha kibao kitakachoonesha wanafunzi waliofaulu vizuri pamoja na walimu waliofaulisha masomo husika ili kuleta ushindani kwa wanafunzi pia kuleta morale ya kufundisha kwa walimu, pia kuwa ni kumbukumbu na kuwathamini wanafunzi na waalimu wanaofanya vizuri.
►Kuwa na malengo kuanzia ngazi ya shule,kata hadi wilaya
Katika agizo hilo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameagiza halmashauri kuhakikisha shule zote za msingi na sekondari zinakaa pamoja kuweka mbinu za kufikia malengo ya shule,kata na hata wilaya katika kuinua hali ya ufaulu Mkoani Mtwara, “ Bila malengo hatuwezi kufika popote” Alisisitiza
►Suala la kumaliza Mtaala wa masomo (Syllabus)
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewataka waalimu wote wa shule za msingi na Sekondari ambao wanafundisha madarasa ya mitihani( Yaani darsa la Nne na Saba kwa shule za msingi na Kidato cha Pili na Nne kwa shule za Sekondari) kuhakikisha wanamaliza Mtaala wa masomo yao (Syllabus) ifikapo mwezi Juni na baada ya hapo wahakikishe wanawafanyisha mitihani mitatu yenye hadhi ya mitihani ya kitaifa ili kuwajengea uwezo na utyari wanafunzi katika mitihani yao ya taifa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.