Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed mapema leo hii afungua kikao cha kwanza cha maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika ukumbi wa Boma Mkoani Mtwara, Ambapo amesema. Nawapongeza sana kwa kazi kubwa tuliyoifanya pamoja kama Mkoa, iliyopelekea Mkoa wetu kuandika historia mpya na ya kipekee kwenye uzinduzi wa Mbio hizi kwa miaka ya hivi karibuni.
Mkoa wa Mtwara utapokea Mwenge wa Uhuru tarehe 30 Mei 2024 toka Mkoa wa Lindi na kuukabidhi tarehe 08 Juni 2024 Mkoani Ruvuma.
Aidha, Kanali Ahmed amesema, kuanzia Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu 2024, Mikoa mitatu (3) bora itakayofanya vizuri itakabidhiwa tuzo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkoa utakaoshika nafasi ya mwisho utapokea cheti cha utendaji usioridhisha. Hivyo basi sisi kama Mkoa tumeona tuanze kuchagiza kasi ya maandalizi ili tuwe sehemu ya Mikoa mitatu itakayopokea Tuzo kwa kutoa zawadi za vyeti kwa Halmashauri tatu (3) zilizofanya vizuri kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 zikiongozwa na Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Kanali Ahmed akamalizia kwa kusema, Kikao hiki kituwezeshe kuhakikisha tunainuka na kusonga mbele tukiwa na nguvu mpya kwa mwaka huu, natumaini tutakitumia vyema kufanya majadiliano chanya na kujipanga ipasavyo kufanikisha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu 2024.
Machi 7, 2024.
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.