Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kanali Ahmed Abbas Ahmed afungua kikao maalum cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania, Tawi la Mtwara.
Watendaji kutoka Halmashauri mbalimbali Mkoani Mtwara wametakiwa kutumia kikao maalum cha kamati ya ushauri cha Mkoa huo kwa mwaka 2024 (RCC) kujadili na kutoa ushauri ili kuboresha mipango na bajeti.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas ndiye aliyetoa wito huo akiwa kwenye kikao hicho cha RCC kilichofanyika leo, Jumanne Machi 5.2024 kwenye ukumbi wa BOT uliopo Manispaa ya Mtwara Mikindani Katika kikao hicho kilicholenga kujadili ajenda moja maalum kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa nusu mwaka wa fedha 2023/2024.
Kanali Ahmed amesema pamoja na majadiliano hayo lakini yapo mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji huo, hivyo amewataka wajumbe kujadili pamoja na kupata ushauri ili kuboresha mipango na bajeti husika
Aidha, Kanali Ahmed ametoa rai kwa watendaji wa Halmashauri zote Mkoani humo kuwajali walioko juu na chini yao ili waweze kukamilisha malengo yanayokusudiwa kwenye maeneo yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.