Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustin Ndugulile akimkabidhi Said Akili, mwanachama wa chama cha Msingi Nyundo B, kijiji cha Nyundo, Halmashauri ya Wilya ya Nanyamba kadi ya uanachama wa Bima ya Afya (Ushirika Afya) mara alipotembelea katika Ofisi za Bima ya Afya (NHIF) mjini Mtwara jana Februali 26, 2019.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea na taratibu za kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma ya Bima ya Afya. Akizungumza jana wakati wa ziara ya kikazi mjini mjini Mtwara Naibu Waziri wa Afya Mhe. Faustin Ndugulile amesema lengo lao ni kuhakikisha mwaka huu 2019 zoezi hilo muhimu kwa afya ya watanzania linatekeklezwa.
“Kubwa ambalo serikali tumepanga kulifanya mwaka huu ni kuhakikisha kila mtanzania anapata Bima ya Afya. Hili ni agizo la Mheshimiwa Rais kuhakikisha kila mtanzania hahangaiki na huduma ya afya na badala yake atembee na kitambulisho kinachomuwezesha kupata huduma hiyo.” Amesema Mhe. Ndugulile
Amesema hadi sasa serikali imeendelea na maboresho katika huduma mbamimbali za Bima ikiwemo CHF iliyoboreshwa inayomuwezesha mwanachama kupata huduma ya afya kwenye vituo mbalimbali tofauti na ile ya awali ambayo ilikuwa ikimuwezesha mwanachama kupata huduma kwenye kituo kimoja tu.
Pia huduma ya Ushirika Afya ambayo inalenga kuwafikia wakulima walioko katika vyama vya ushirika vya mazao mbalimbali. Mheshimiwa Naibu Waziri amempongeza ndugu Said Akili, mkulima wa korosho kutoka kijiji cha Nyundo katika chama cha Msingi Nyundo B kwa kutambua umuhimu wa Ushirika Bima na kujiunga. Aidha amesema Ushirika Bima inapatikana kwa shilingi 76,800 kwa mwaka na inamuwezesha mwanachama kupata huduma ya afya kwenye vituo zaidi ya elfu sita nchi nzima.
Amesema hizi huduma zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto za huduma za afya. Kinachotakiwa sasa ni kuhamasiha wananchi kujiunga na bima hizi kwani zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na changamoto hizi.
Kwa upande wake Said Akili amewataka wakulima wenzake kuchangamukia huduma hiyo kwani changamoto za wakulima ni ninyingi.
“Wakulima wengi tunatumia jembe la mkono na Panga na tunakuwa na fedha kipindi cha miezi ya mauzo. Baada ya hapo wengi tunakuwa hatuna fedha. Bahati mbaya ugonjwa hauchaguai muda hivyo ukiwa na kadi ya Bima itasaidia kupata huduma ya afya bila wasiwasi”. Amesema Said
Mhe. Ndugulile amekuwa na zira ya siku mbili mkoani hapa ambapo ametembelea maeneo mbalimblai ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula, Hospitali ya Kanda ya Kusini inayojengwa mjini Mtwara, Ofisi za Bandari Mtwara pamoja na ofisi za Bima ya Afya Mtwara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.