Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atawasili mkoani Mtwara tarehe 2 April 2019. Pamoja na miradi mingine mingi atakayotembelea na kuzindua, ataweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin.
Kiwanda hiki ni matunda ya ziara yake ya kwanza mkoani Mtwara aliyoifanya kuanzia tarehe 3 hadi 5 Machi 2017. Ujio wa Mheshimiwa Rais uliamsha ari ya wawekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo viwanda vya kubangua korosho na Kiwanda cha Yalin atakachokitembelea ni ushuhuda wa hilo.
Kabla ya ziara ya Mheshimiwa Rais ya Machi 2017 kulikuwa na malalamiko kutoka kwa mwekezaji wa kiwanda cha cha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote. Dangote alikuwa akilalamika kutopata ushirikiano wa kupata kibali cha kuweka miundmombinu itakayomuwezesha kuzalisha saruji kwa kutumia umeme wa gesi asilia. Aidha, upatikaji wa makaa ya mawe kutoka mchuchuma nao uliingia ukakasi na hivyo kutishia kufungwa kwa kiwanda.
Ujio wa Mheshimiwa Rais ulitatua changamoto zote kwa haraka na hivyo kurudisha imani ya wawekezaji siyo tu kwa Mkoa wa Mtwara bali kwa nchi nzima. Mheshimwa Rais aliagiza ndani ya siku saba Dangote awe amepewa eneo la makaa ya mawe huko Mchuchuma na TPDC wahakikishe gesi inafikishwa kwenye Kiwanda cha Dangote.
Maamuzi hayo ya Mheshimiwa Rais yalidhihirisha utekelezaji wa kauli yake ya kuwa na Tanzania ya viwanda kwa vitendo na ya uchumi wa kati ifikapo 2025 na kutoa imani kwa wawekezaji wengine.
Bwana Zhu Xiufeng Raia wa China akachangamkia uwekezaji kwa kujenga Kiwanda cha kubangua korosho chenye uwezo wa kubangua tani 10,000 kwa mwaka mitambo yote itakapokamilika kufungwa. kwa sasa kiwanda kina uwezo wa kuzalisha kuanzia tani 27 hadi 30 kwa siku na tani 6,000 kwa mwaka.
Video ya tukio zima hii hapa https://www.youtube.com/watch?v=BVl8APMXzMg
Unaweza kupata video zote za ziara hiyo katika maeneo sita aliyotembelea kwa kuingia kwenye tovuti ya Mkoa wa Mtwara www.mtwara.go.tz au tembelea youtube channel ya Mtwara rs. Usisahau ku-subscribe
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.