Kanisala Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kusini Mashariki Usharika waKanisa Kuu wamemtunuku Tuzo ya Mwanamke Jasiri Mkuu wa MKOA wa Mtwara. Mhe.Halima Dendego ikiwa ni kutambua mchango wake Mkubwa ktk kusukuma maendeleo yaMtwara.
Tuzohiyo iliyotolewa Jana katika kanisa la KKKT lililoko Mjini Mtwara lilishuhudiwana viongozi mbalimbali wa mkoa pamoja na waimbaji kutoka makanisha mbalimbaliikiwemo kwaya ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtwara.
Akizungumzawakati wa kumkabidhi tuzo hiyo, Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Lucas MbeduleJuda amesema vipo vielelezo vya mambo mengi makubwa aliyoyafanya Mhe.Dendego ambayo ni kielelezo cha ujasiri wake katika kusimamia haki.
Amesemayeye mwenyewe Askofu amekuwa mfuatiliaji wa karibu wa kazi za Mheshimiwa Mkuuwa Mkoa tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga kabla ya kuhamishiwa hapa Mtwaramiaka mitatu iliyopita.
Akinukuumaandiko matatatifu kutoka kwenye kitabu cha “Marko 16.1-4 Mbedule amesema kitabuhicho kinaonesha ujasiri mkubwa unaohitajika katika kuitafuta haki jambo ambaloMheshimiwa Dendego ameliweza.
“Hatasabato ilipokwisha kupita, mariamu Magdalena na Mariamu mamaye Yakobo, naSalome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Hata alfajili mapema siku yakwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza. Wakasemezana waokwa wao, ni nani atakayetuviringishia lile jiwe mlangoni pa kaburi? Hatawalipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuviringishwa, nalo lilikuwakubwa mno.”
Anasemaandiko hilo linawataja baadhi ya watu ambao ni maarufu kwa kukatisha tamaa wenzaokatika jitihada za mapambano ya ukombozi kama ambavyo mmoja wa wanawake hao alivyojaribukuwakatisha tamaa wanawake wenzake lakini ujasili wa wale akina mamahaukukatishwa tamaa katika kuliendea jiwe lililofunika mwili wa Yesu.
Akizungumziahati aliyoitoa Askofu Mbedule amesema hati hiyo inatambulika kama HATI YAASKOFU YA HESHIMA YA JUU ambayo hutolewa Mara chache, kwa watu wachache hasabaada kujiridhisha na utendaji uliotukuka kwa mhusika.
Kwaupande wake Mhe. Dendego ambaye amekuwa Mkuu wa MKOA huu kwa miaka mitatu sasaanasema tuzo hiyo imempa nguvu ya kuendeleza jitihada zake kutetea maslahi yawengi hasa wanyonge. Amesema wapo watu wengi ambao wamekuwa wakimkatisha tamaakatika jitihada zake. Wengine wamekuwa wakimbeza na hata kumsingizia vitu vingilakini kwa heshima aliyopewa na kanisa hilo imempa nguvu na anajiona ni mpyakatika mapambano.
MheshimiwaDendego amewataka akina mama wengine wajipe moyo wa mapambano kwani katikakufikia ushindi lazima mtu ajitowe mhanga.
Kwaupande wao wananchi waliokuja kushuhudia tukio hilo wamepongeza uamuzi wakanisa hilo kwamba umefanyika katika muda muafaka na kwa usahihi kabisa.
MwalimuFrank Komba wa shule ya Msingi magomeni Mkoani Mtwara anasema amekuwaakifuatilia kwa karibu kazi za Mkuu wa Mkoa tangu amekuwepo hapa naamefurahishwa na mambo mengi likiwemo suala la kusimamia elimu huku akiwabanawananfunzi wanaopata ujauzito na wanaowapa. Anamshauri Mkuu huyo aendelee najitihada hizo kwani nidhamu kwa wanafunzi imejengeka sasa.
JosephHaule Mkazi wa Mangamba Mtwara mjini anaongeza kuwa Mkuu wa Mkoa ameweza kuzuiasuala la kuwatumikisha watoto wa kike katika mtindo wa wafanyakazi wa ndani nahata wakati mwingine kuwageuza chombo cha starehe. Amemtaka Mheshimiwa Magufuliaendelee kumuunga mkono na asimuhamishe mkoani Mtwara.
AidhaViktoria Daudi mkazi wa Mtwara anaguswa na kazi za Mkuu wa Mkoa katika suala lausimamizi mzuri wa zao la Korosho. Anasema kabla yake kulikuwa na ukiukwaji wataratibu za ununuzi na uuzaji wa korosho ambapo wanunuzi wengi walikuwa wakinunuakorosho katika mfumo usio rasmi na hivyo kuwanyima mapato stahili wakulima. Baadaya usimamazi wa Mheshimiwa Dendego suala hilo limepungua kwa kiasi kikubwa nasasa wananchi wanafurahia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.