Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali amezitaka klabu za wapinga rushwa shuleni ziige mfano kutoka shule ya sekondari Ndanda. Amesema klabu nyingi walizokutana nazo katika mikoa waliyopitia zilikuwa zikijihusisha sana na shughuli ya kutoa elimu kwa jamii tofauti na Klabu hiyo ambayo imeenda mbali zaidi katika mapambano hayo.
vijana hao wamemweleza Mkimbiza Mwenge huyo kwamba wanamiradi ya kilimo, ufugaji, utengenezaji wa tofari pamoja na sanaa za utamaduni ambavyo vyote kwa pamoja wamekuwa wakivitumia kuongezea kipato kwa Klabu na wanakikundi.
“Huu ni mkoa wa 30 kati ya mikoa 31 ambayo tunatarajia kuikamilisha hivi karibuni, lakini klabu ya aina hii hatujawahi kuiona. Klabu nyingi tulizokutana nazo zimejikita katika kuelimisha. Si vibaya kuelimisha lakini hawa wamekuja na mbinu mbadala ya kuondokana na mawazo mgando yanayoweza kuwafanya wakawa na fikra potofu katika jamii Klabu zingine zinapaswa kuiga mfano huu”. Amesema Mzee.
Klabu hiyo inayoundwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita katika shule hiyo wameanzisha kilimo cha korosho, Nyanya, Ndizi na Ufugaji wa kisasa. Pia hujishughulisha na michezo ya utamaduni kwa lengo la kutunza asili ya mwafrika.
Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake mkoani Mtwara ambapo leo ulikuwa katika siku ya 3 kati ya siku 9 unazotegemea kukimbizwa mkoani Mtwara.
Kaulimbiu ya mwenge wa Uhuru mwaka huu ni “Maji ni haki ya kila mtu. Tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi Mkuu wa serikali za Mitaa”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.