Bei ya korosho msimu wa 2017 imeendelea kupanda mkoani Mtwara huku ikivunja rekodi ya tangu zao hili kuwepo hapa Mkoani. Katika minada iliyofanyika leo mkoani hapa bei ya juu ya korosho imeuzwa shilingi 4,007 kwa kilo wakati bei ya chini ikiwa shilingi 3880.
Bei ya juu ya korosho iliyowahi kufikiwa mkoani hapa ni ilitokea msimu wa 2016/2017 ambapo bei ya juu ya korosho ilifikia shilingi 4000 wakati uzalishaji ukiwa umepanda hadi kufikia tani 172,771.109 tofauti na tani 106,940.222 zilizokuwa zimezalishwa msimu wa 2015/2016.
Akizungumza na mwandishi wetu Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mtwara anaeshughulikia uchumi na uzalishaji, Amani Lusake amesema katika mnada uliofanyika katika kijiji cha Mihambwe leo Chama cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU) kimeuza tani 10,000 ambapo bei ya juu ya korosho imeuzwa kwa shilingi 4,007 wakati bei ya chini ni shilingi 3970.
Kwa upande wa Chama cha Ushirika cha Masasi na Mtwara (MAMCU) zimeuzwa tani 16,831.7 ambapo bei ya juu imefikia shilingi 3985 wakati bei ya chini ikiwa ni shilingi 3880.
Bei hii ya korosho ni alama na hatua muhimu ya mafanikio katika kilimo cha Korosho ambacho ni muhimu kwa maendeleo ya Mkoa wa Mtwara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.