Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman amesema kuwa serikali ipo tayari kuyasikiliza maoni ya wananchi ili kuboresha mwenendo wa utendaji katika sekta ya sheria kwa kufanya maboresho ya kiutendaji kupitia maoni na mitazamo yao.
Mhe. Jaji ameyasema hayo alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na kusisitiza kuwa wakati wa kutatua changamoto zilizoshindikana katika mifumo ya sheria umewadia jambo litakaloongeza imani ya wananchi.
Pia ameongeza kuwa kazi kubwa itakayofanywa katika ziara yake ni kutafuta taarifa sahihi zinazohusiana na utendaji wa Taasisi za haki jinai kwa kuwafikia wananchi wenyewe na kuzungumza nao.
“Tunataka taarifa ya ripoti yetu ikaguse uhalisia wa maisha ya mtanzania ili sasa mapendekezo na mapungufu tutakayoyapata yakatatue kabisa kero zilizopo juu ya michakato ya kiutendaji katika usimamiaji wa sheria” aliongeza Jaji Chande.
Kwa upande wake Kanali Abbas ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuwasikiliza wananchi na kupata maoni yao kwani ni njia itakayoboresha mchakato wa upatikanaji wa haki hasa katika taasisi zinazosimamia sheria na utawala bora.
Ziara hiyo inayoshirikisha timu yenye wajumbe11 inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande inalenga kufanya tathimini ya utendaji katika taasisi za sheria sambamba na kukusanya maoni na taarifa zitakazosaidia kufanya maboresho katika mfumo wa utoaji haki / Sheria na Haki Jinai.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.