Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Mtwara katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa mapema mwaka 2015 (Picha kutoka Maktaba).
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mji wa Mtwara. Zoezi hili linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Boma Mkoa ulioko Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mei 2, mwaka huu kuanzia saa 2 asubuhi.
Akielezea mikakati ya zoezi hilo Afisa MipangoMiji mkoa wa Mtwara Bi, Janepher Shadrack Kimaro amesema maandalizi yamekamilika, hivyo awataka waalikwa wote kujitokeza kwa wingi.
Amaesema mpango huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na uongozi wa Mkoa na halmashauri mbili za Manispaa ya Mtwara Mikindani na Halmashauri ya Wilaya Mtwara, unakusudia kukidhi mahitaji ya kukua kwa mji wa Mtwara kwa miaka 20 kuanzia 2015. Mpango huu unajumuisha hekta 95,117 ambazo ni eneo lote la Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata 9 za Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara. Aidha idadi ya watu walio kwenye eneo hili la mpango kwa sasa ni 170,000, katika kipindi cha miaka 20 mpaka 2035 idadi ya watu inatazamiwa kuongezeka na kufika 1.7milioni.
Kuhusu lengo na maono ya mpango huo ni kuhakikisha kuwa kufika mwaka 2035 Mtwara kinakuwa kituo muhimu cha uwekezaji na kitovu cha huduma na shughuli muhimu za usafiri na usafirishaji katika ukanda wa mikoa ya kusini mwa Tanzania hususani mikoa ya Lindi, Mtwara Ruvuma na Njombe na ukanda wa maendeleo wa Mtwara ambao unahusisha nchi za Tanzania, Msumbiji, Malawi, Zambia na Afrika ya kusini. Pia kuifanya Mtwara kuwa Jiji lenye ustawi wa maisha shindani na majiji yaliyo kwenye ukanda wa bahari ya hindi, mashariki na kusini mwa Afrika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.