Maafisa waaandikishaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wametakiwa kuzingatia misingi ya haki na sheria katika kuwaandikisha wapiga kura. Rai hiyo imetolewa leo Januari 3, 2020 na Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Balozi Omari Mapuli wakati wa semina fupi ya mafunzo ya uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura iliyofanyika ukumbi wa Boma Mkoa Mkoani Mtwara
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki hivyo uandikishaji ni hatua muhimu inayotakiwa kuzingatia misingi hiyo.
“Zoezi hili ni zoezi ambalo linaendeshwa kwa mjibu wa sheria, kanuni pamoja na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, hivyo pamoja na uzoefu wa siku za nyuma ni vema kuzingatia mafunzo ili tukatekeleze zoezi ipasavyo na katika muktadha wa sasa.” Amesema Mapuli
Amesema zipo changamoto ambazo zilibainishwa kutoka kwa wandikishaji wasaidizi pamoja na waandishi wasaidizi wa BVR Kit ambazo ni pamoja na kutokufuata ama kutozingatia ratiba ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura iliyotolewa na Tume, pia kutokufanya mandalizi ya mafunzo mapema suala ambalo linapelekea kufanya mafunzo kukosa ufanisi uliokusudiwa.
Changamoto zingine ni kutozingatia maelekezo ya utunzaji wa vifaa.
Aidha, amewahakikishia kuwa serikali ya Mkoa ambako zoezi hilo linatekelezwa imejipanga kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa.
Mafunzo haya yaliwahusisha Maafisa Waandikishaji, waandikishaji Wasaidizi, Maafisa wa Uchaguzi ngazi ya halmashauri pamoja na Maafisa TEHAMA huku zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura likitarajiwa kufanyika kuanzia Januari 12 hadi 18, 2020.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.