Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha akizungumza na Wakuu wa Shule zenye kidato cha sita mkoani Mtwara katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara Agosti 15, 2018
Naibu Waziri wa Elimu Mhe. William Ole Nasha amewataka viongozi wa Mkoa wa Mtwara kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana katika idara ya elimu yanaendelezwa. Amesema mkoa wa Mtwara ulikuwa ukiripotiwa kuwa na matokeo mabaya kielimu jambo ambalo lilikuwa likitoa taswira isiyo nzuri kwa jamii lakini matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018 ambayo mkoa wa Mtwara umekuwa wa kwanza kitaifa yameleta tafsiri inayoonesha kuwepo kwa jitihada kubwa za kufuta hisia hizo.
Mheshimwi Nasha ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Wakuu wa Shule za Sekondari zenye kidato cha sita mkoani Mtwara.
Nasha ambaye alikuwa na ziara ya siku mbili mkoani hapa amesema hakuna jambo linaloshindikana kunapokuwawepo na jitihada za dhati za kulishughulikia. Jambo la msingi ni uongozi wa dhati uliodhamiria kuondoa changamoto husika.
“Hakuna kinachoitwa kufaulu kwa coincidence. Haitokei bahati mbaya. Ni kama kulivyo kufeli. Wanafunzi wakifeli lazima kuna sababu. Sababu hiyo inaweza kuwa na mambo mengi lakini uongozi unahusika”.
Mheshimiwa Nasha ameendelea kwamba, “kulipo na ufaulu. Kuna jitihada za viongozi. Kuna watu wamefanya hiyo kazi. Ndiyo maana leo hii nafurahi sana kuja kukutana na nyie Wakuu wa Shule za A-level za mkoa wa Mtwara. Pamoja na viongozi mlioko hapa. Kuja kusema serikali inatambua na inawapongeza kwa jitihada kubwa ambayo mmeifanya na kuleta ufaulu wa kihistoria katika mkoa wa Mtwara”.
Akizungumzia mafanikio hayo Mkuu wa shule ya sekondari Ndanda Mwalimu …. amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa dhati kwa wadau wote wa elimu mkoani hapa ikiwemo mikakati binnafsi ya shule katika kufikia lengo.
Pamoja na mikakati ya kimkoa bado tulikuwa na mikakati ya kishule ambayo ilimhusisha si mwanafunzi tu bali hata walimu na wafanyakazi wengine pamoja na jamii inayotuzunguka ambayo ilihusika kuhakikisha nidhamu ya watoto inakuwa nzuri.
Kwa upande wa ndani tuliutangaza mwaka 2018 kama mwaka wa taaluma ambapo kila department ilikuja na mikakati ya kitaaluma ambayo ililenga kuondoa division 0 na 4 na kila somo kuondoa daraja F na S. Pia tulilenga kuhakikisha shule inatoka nafasi ya 200 inaingia kwenye Mia moja bora”. Amesema ….
Kwa upande wake, Afisa Elimu Mkoa, Germana Mung’aho amesema mkoa uliamua na kudhamiria kuondoa madaraja sifuri. Uongozi wa mkoa ulifanya vikao ambavyo viliwahusha wadau mbalimbali wa elimu ambao waliweka mikakati mingi ikiwemo kumaliza mtaala mapema na kutoa motisha kwa walimu.
Amesema kwa sasa mkoa unasimamia kaulimbiu ya “Mtwara is a zero Free zone in Form Six Results. Play your part” ambayo lengo lake ni kuakikisha ufaulu unalindwa.
Mheshimwa Nasha alikuwa na ziara ya siku mbili Mkoani Mtwara ambapo alitembelea vituo mbalimbali ikiwemo shule ya usekondari ya Ufundi Mtwara, Chuo cha Ufundi VETA , Chuo cha Ualimu Kitangari na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Newala.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.