Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Masasi wamefanya maandamano ya amani kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya kusimamia rasilimali za Tanzania.
Maandamano hayo yaliyofanyika leo yakianzia Ofisi za Chama cha Mapinduzi wilaya ya Masasi na kuishia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi yalipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mheshimwa Seleman Mzee.
Akizungumza baada ya kupokea maandamano hayo Mheshimiwa Mzee amesema kazi nzuri inayofanywa na Mheshimwai Magufuli inastahili pongezi kwa kila mtanzania mwenye kuitakia mema Tanzania, amewasifu vijana hao na kuwataka wawe mstari wa mbele kusimamia maagizo yanayotolewa na Mheshimiwa Rais pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi, Alfred Mwambeleko amesema wameamua kufanya maandamano hayo kutokana na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Mheshimwia Rais katika kusukuma mbele maendeleo ya Nchi. Amesema wao kama sehemu ya kundi ndani ya Chama cha Mapinduzi wameona busara kuungana na watanzania wengine katika kumpongeza Mheshimwa Rais hasa katika ushujaa aliouonesha kuzuia usafirishaji wa Makinikia kwenda nje ya nchi na hatimaye kamati alizoziunda kugundua wizi mkubwa wa rasilimali za nchi.
Amesema umoja wa vijana Masasi wako pamoja naye na wanamtakia mapambano mema.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi Mzee Kazumari amesema Vyama vya upinzani vinavyobeza jitihada za Mheshimiwa Magufuli vinapoteza muda. Amesema kwa jinsi Mheshimiwa Rais anavyoendesha nchi vyama vya upinzania havina haja ya kuwepo bali kuungana na CCM ili kusuma maendeleo ya Nchi.
Kuangalia Video yake Bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.