Na Joina Nzali. Afisa Habari Masasi DC
Tatizo la wananchi wengi wa kata zilizopo pembezoni mwa mto Ruvuma katika halmashauri ya wilaya ya masasi kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na mamba wanaopatikana katika mto huo linatarajiwa kuisha baada ya mradi wa maji unaotekelezwa kutokana na chanzo mto huo kukamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Mhandisi wa maji wa halmashauri hiyo Mhandisi Francis Bwire wakati akikagua utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 2.7 ambao unatarajia kusambaza maji katika vijiji 8 vyenye jumla ya watu 17420 ndani ya kata ya chikolopola na Mnavira.
Amesema kuwa wananchi wa kata hizo kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitegemea mto Ruvuma kupata huduma ya maji kwa matumizi mbalimbali hali ambayo imekuwa ikipelekea wananchi wengi kujeruhiwa au kuuawa na mamba wakati wa kuchota maji na shughuli zingine, hivyo mradi huu utaondoa kabisa tatizo hili kwa kuwa wananhawatahitaji kupata huduma ya maji mtoni bali watapelekewa katikamaeneo yao.
“watu wengi wamepoteza maisha huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu uliosababishwa na mamba wanaopatikana katika mto Ruvuma” alisema Bwire.
Bwire amesema utekelezaji wa mradi huo hadi sasa upo asilimia 70 ambapo ujenzi wa matenki mawili yenye ujazo wa lita 100,000, ukarabati wa tanki 1 lenye ujazo wa lita 25,000, ujenzi wa vituo 38 vya kuchote maji, ulazaji wa bomba kubwa kilimita 12 na dogo kilomita 9 umekamilika na ujenzi wa chanzo unaendelea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.