Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 zimebisha hodi Mkoani Mtwara Leo Mei 17,2025 ambapo unatarajiwa kuzindua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi yenye thamani ya zaidi Shilingi Bilioni 18.3
Mara baada ya kuwasili Mkoani Mtwara Mwenge wa Uhuru ulianza kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu ambapo uliweka jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya maji katika Kijiji cha Michiga na baadae kukagua na kuona shamba la miti la mfano katika Kijiji cha Chinyanyira wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 33.8.
Halikadhalika Mwenge wa Uhuru katika siku yake ya kwanza Mkoani Mtwara uliweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa Mradi wa vyumba vya madarasa na Ofisi za walimu uliogharimu Shilingi milioni 55.35.
Na baadae Mwenge wa Uhuru Ulikagua na kuona Mradi wa kikundi cha vijana cha usafirishaji abiria boda boda na baada kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya Namaguruvi na kuhitimisha siku yake ya kwanza Kwa kuweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa barababara ya msangi na Jerome Kwa kiwango cha lami yenye thamani ya Shilingi milioni 755.2.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.