Leo Juni 8,2024 Serikali ya Mkoa wa Mtwara imekabidhi Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Sauti moja Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya kuendelea na mbio zake mkoani humo.
Akizungumza mkoani Ruvuma kwenye kukabidhi Mwenge huo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Kenan Sawala amesema Mwenge umepitia miradi 62 mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 30 ukiwa mkoani Mtwara.
Pia umekimbizwa katika njia zenye urefu wa kilomita 906.6 kwenye Halmashauri zote 9 na kuweka mawe ya msingi miradi 22, kufungua miradi 2 na kuzindua miradi 11.
Aidha, Mwenge umeona na kukagua miradi 27 inayotekelezwa na wananchi kwa kushirikiana na Serikali Kuu, wahisani, pamoja na Halmashauri kuwa ujumla.
"Miradi hii yote iliyokamilika na mingine mingi ambayo inaendelea katika mkoa wetu ni kazi kubwa ya Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan, sisi kama Mtwara tunashukuru sana kwa kutupatia fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya mkoa wetu."amesema Kanali Sawala.
Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava ameridhika na utekelezaji wa miradi katika mkoa huu wa Mtwara na kupongeza namna ambayo fedha nyingi zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji huo zilivyotendewa haki.
Aidha, amewataka viongozi kuendelea kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo bado haijakamilika na tayari imewekwa jiwe la msingi ili iweze kukamilishwa vizuri.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema Mwenge ukiwa mkoani humo utakimbizwa katika Halmashauri 8 na kutembelea miradi 72 mbalimbali ya maendeleo nyenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 46.
Pia utakimbizwa umbali wa kilomita 1289.50 na utafungua miradi 17, miradi 13 kuwekewa mawe ya msingi na miradi 42 itatembelewa, kukaguliwa.
Aidha Mwenge huo kwa mkoa wa Mtwara ulipokelewa Mei 30,2024 katika kijiji cha Mpapura Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na Juni 7, mwaka huu umemaliza mbio zake ndani ya mkoa huo.
ASANTE NA KILA LA KHERI MWENGE WA UHURU 2024.
Juni 8, 2024.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.