Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Mtwara Leo tarehe 1 Juni 2024 umeanza ziara yake katika Halmashauri ya Mji Nanyamba Wilayani Mtwara.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri hiyo umeweka jiwe la msingi, umezindua pamoja na kutembelea na kuona jumla ya Miradi 7 yenye thamani ya shilingi Bilioni 7.73
Mradi wa kwanza ulikuwa mradi wa vyumba viwili vya madarasa wenye thamani ya shilingi Milioni 48.3 katika shule ya msingi Maranje.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mradi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. Godfrey Mzava ameipongeza Halmashauri ya Mji Nanyamba kwa kusimamia vizuri matumizi ya mfumo mpya wa Manunuzi wa NEST na kusema kuwa unasaidia kuondoa mianya ya ubadhilifu na upendeleo katika utoaji zabuni.
Mara baada ya zoezi Hilo Mwenge wa Uhuru ulielekea Kijiji Cha Chawi kukagua shamba la Miti la mjasiliamali . Saada ni Nankaha ambapo Mhe. Godfrey Mzava amewataka viongozi na wadau wa Mazingira kuhakikisha wanahamasisha wananchi kupanda miti Ili kutunza Mazingira kama kauli mbiu ya Mwenge ya mwaka huu inavyosisitiza.
"TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU"
Mradi mwingine uliotembelewa na Mwenge ni mradi umeme wa REA ambapo kiongozi wa Mwenge alikagua na kuona zoezi la uwashaji wa umeme eneo la Chawi sokoni katika nyumba ya mzee Mohamed Hamis ambapo alishiriki kuwasha umeme katika nyumba hiyo, zoezi linaloashiria umuhimu wa Serikali kuwekeza shilingi Bilioni 22 kusambaza umeme katika vijiji vya Halmashauri ya Mji Nanyamba huku akiwataka wananchi kuitunza Miundombinu ya Mradi huo.
Akiwa katika shule ya msingi Chawi Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mh. Mzava alikagua na kuona shughuli za Banda la Mazingira, alikagua Banda la Afya na Lishe pamoja na kuzindua klabu ya wapinga rushwa.
Kisha Mwenge wa Uhuru ulikagua hatua ya Mradi wa uendelezaji wa Zahanati Mkomo katika Kijiji Cha Mkomo Uliogharimu kiasi Cha shilingi Milioni 9.9.
Akiwa katika Zahanati hiyo kiongozi wa Mbio za Mwenge Mhe. Godfrey Mzava ameiagiza Halmashauri hiyo kukamilisha Ujenzi wa Miundombinu ikiwemo kuweka mfumo wa kuvuna maji ya mvua pamoja na kujenga kichomea taka Ili kurahisisha mchakato wa utoaji huduma.
Katika mtaa wa Kilimanjaro katika Mji wa Nanyamba Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la katika Mradi wa Ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa moja uliopewa jina Hawa Ghasia Road Uliogharimu kiasi Cha shilingi Milioni 450.
Katika Mradi huo Mhe. Mzava ameutaja kuwa ni kielelezo jitihada za Serikali katika kuboresha Miundombinu ya usafirishaji na kuwataka wananchi kuitunza barabara hiyo.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. Godfrey Mzava ameipongeza Wakala wa Barabara Vijijini TARURA kwa kukidhi vigezo vya mfumo Mpya wa Manunuzi NEST kama ambavyo sheria inawataka na kusema kuwa hicho ni miongoni mwa vigezo ambavyo vimechangia kufanikisha utekelezaji wa Mradi huo.
Juni 01, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.