Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeingia siku ya pili Mkoani Mtwara ambapo Leo ni zamu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Jumla ya Miradi 6 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1 imewekewa mawe ya msingi huku mingine Ikitembelewa.
Ukiwa katika Kata ya msimbati Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika kituo Cha Afya msimbati Mradi ulioghari kiasi Cha shilingi Milioni 618.9
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Mhe. Godfrey Mzava amememwagiza Katibu Tawala Mkoa kuunda timu ya Ukaguzi maalumu Ili kujiridhisha kuhusu matumizi ya Fedha za Mradi huo.
Uamuzi huo wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mhe Godfrey Mzava unafuatia kutoridhishwa na nyaraka za matumizi ya fedha za mradi ambapo ametoa siku Saba kwa Uongozi wa Mkoa kukamilisha Ukaguzi Maalumu Ili kupata ukweli wa swala hilo.
Halikadhalika katika Kata hiyo ya Msimbati Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Msimbati Uliogharimu kiasi Cha shilingi Milioni 141.8.
Mradi mwingine uliowekewa jiwe la msingi ni mradi wa maji Makome katika kijiji Cha Makome Uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 600 ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 70.
Kuhusu utekelezaji wa Mradi huo Mhe. Mzava amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kuongeza kuwa inatoa jibu la changamoto ya Maji iliyokuwa inawakabili wakazi wa eneo hilo.
Halikadhalika Mhe. Godfrey Mzava ameipongeza Mamlaka ya Usambazaji wa Maji Safi Vijijini na Usafi wa Mazingira RUWASA kwa kuzingatia sheria ya Manunuzi kupitia matumizi ya mfumo Mpya wa NEST na ambapo amezitaka taasisi nyingine kuitumia mfumo huo kama sheria Inavyoelekeza.
Mei 31, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.