Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Mkoani Mtwara leo 04 Juni 2024 zimeingia katika siku yake ya Sita ambapo hapo jana umebisha hodi katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Katika Halmashauri hiyo Mwenge wa Uhuru umeimulika Miradi 9 yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.6.
Ziara ya Mwenge wa Uhuru mapema asubuhi ilianzia katika Kijiji Cha Makukwe ambako kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mhe. Godfrey Mnzava alikagua na kuona Maendeleo ya klabu ya kuzuia na kupambana na rushwa katika shule ya sekondari Makukwe.
Kisha Mwenge wa Uhuru ukaelekea katika Kijiji Cha Mango ambako umeweka jiwe la msingi katika zahanati ya Kijiji hicho.
Baada ya zoezi hilo Mwenge wa Uhuru ulielekea Kijiji cha Nanda ambako ulikagua na kuona jitihada za zinazofanywa na Serikali kusambaza huduma ya Maji Katika maeneo mbalimbali ukiwemo mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 1.
Ukiwa bado unamulika katika Kijiji hicho, Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari ya Nanda Mradi Uliogharimu kiasi Cha shilingi Milioni 568.5.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava ameagiza TAKUKURU na TRA kuwasaka wazabuni waliohusika kutoa risiti hewa katika manunuzi yaliyofanyika wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Pia Mhe. Mnzava ameagiza Halmashauri ya Wilaya kuhakikisha inasimamia marekebisho ya miundombinu yote iliyobainika kuwa na kasoro.
Baada ya hapo Mwenge ulielekea eneo la Kitangari hospitali ambako uliweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 1.13 iliyogharimu kiasi cha shilingi Milioni 649.9.
Mradi mwingine uliofunguliwa katika ziara hiyo ya mbio za Mwenge ni Mradi wa Nyumba ya kulala wageni ya mkulima wa korosho eneo la Kitangari Sokoni yenye thamani ya shilingi Milioni 245 pamoja na kuona na kukagua shughuli za wajasiliamali katika eneo hilo.
Kisha Mwenge ulielekea katika Kijiji Cha Meta ambako kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa alikagua na kuona shamba la Miti ikiwa ni jitihada za kuunga Mkono uhifadhi wa Mazingira.
Mwenge wa Uhuru umehitimisha ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala
Juni 04, 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.